Wasifu wa Kizza Besigye

Kanali (Mstaafu) Dkt Kizza Besigye Kifeefe alizaliwa mwaka 1956 katika wilaya ya Rukungiri, magharibi mwa Uganda.
Besigye alifuzu kama daktari baada ya kusomea Chuo Kikuu cha Makerere, mjini Kampala.
Alijiunga na chama cha Museveni cha Uganda Patriotic Movement muda mfupi baada ya kuondolewa madarakani kwa Idi Amin 1978.
Mwaka 1982, alijiunga na Museveni vitani baada ya kuzuiliwa miezi miwili katika hoteli moja mjini Kampala akituhumiwa kushirikiana na waasi.
Baada ya Museveni kuingia uongozini, alimteua Dkt Besigye, wakati huo akiwa na umri wa miaka 29, kuwa waziri wa nchi aliyesimamia masuala ya ndani na masuala ya siasa za taifa.
Dkt Besigye alipanda cheo jeshini na kufikia cheo cha kanali.
Alistaafu muda mfupi kabla ya uchaguzi mkuu wa 2001, miezi michache kabla ya kujitokeza na kutangaza kwamba angewania urais.

Alipata asilimia 28 ya kura zilizopigwa akilinganishwa na mshindi, Museveni, aliyepata asilimia 69.
Baada ya kushindwa, Besigye aliwasilisha kesi Mahakama ya Juu kupinga matokeo ya uchaguzi. Alipoteza kwenye kesi hiyo na akakimbilia uhamishoni Afrika Kusini akilalamikia kudhulumiwa kisiasa.
Alirejea Novemba 2005 na kuongoza chama cha FDC kwenye uchaguzi wa februari.
Hata hivyo alikamatwa wiki chache baadaye na kushtakiwa mashtaka kadha yakiwemo uhaini na ubakaji.
Aliachiliwa huru wiki mbili baada ya kuanza kwa kampeni za uchaguzi.
Besigye husifiwa sana kutokana na moyo anaoonyesha anapotoa hotuba zake na wengi wamemsifu kwa kusimama na kupinga utawala wa Museveni.
Hata hivyo, wakosoaji wake humshutumu wakisema ana uchu wa madaraka na baadhi husema hawezi kufanikisha mabadiliko yoyote kutokana na uhusiano wake wa muda mrefu na Museveni.
Mke wake ni Winnie Byanyima, mhandisi wa kwanza wa usafiri wa ndege nchini Uganda. Wana mtoto wa kiume.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment