Rapper
na hitmaker wa ‘Nasema Nao’ Ney wa Mitego ameimbia‘exclusively’ Bongo5
kuwa hana mpango wa kumjibu Nikki Mbishi aliyeandika wimbo wa kumdiss
uitwao ‘New wa Mitego’. Miongoni mwa mashairi kwenye wimbo huo yanasema,
“’Ney wa mitego, anagawa ndogo ka gay mwenye pepo’.
Pia
February 6, Nikki alitweet, ‘I am deeply in love with this shawty named
@Nay wa mitego’.Bongo5 imeongea na Ney kuhusiana na issue hiyo ambaye
amesema hana mpango wa kumjibu Nikki kwakuwa anatafuta pa kutokea.
“Anatafuta
pa kutokea mimi sitaki kuongea lolote kuhusu yeye. Mimi sitaki
kufuatilia kwasababu nimeshagundua kuwa ni upuuzi, yeye anatafuta njia
ya kupita mimi sitaki kuzungumza chochote, hata interview yoyote kuhusu
yeye sitaki, yaani nalizungumza hili kwasababu nyinyi ni wanangu
(bongo5) lakini nimekataa, nimekataa kabisa, sitaki kabisa kumzungumzia
huyo mtu,” amesema Ney.
“Kama
kuna wananchi ambao ni matahira wanaweza kuelewa hicho alichokifanya
it’s okay. Mimi huwa namuimba mtu kwa kitu ambacho kila mtu anakiona na
ndio maana nimekuwa na mashabiki wengi sana kwasababu mimi huwa naongea
ukweli. Nikisema Chidi Benz katoboa pua ni kweli katoboa pua, sijawahi
kumuimba mtu kwa matusi au nini kwahiyo siwezi kubishana na mtu wa aina
hiyo. Kwanza hajulikani, hajui anafanya nini, kwanza yeye mwenyewe
hajielewi, kujielewa hakuna mwanaume anasuka hata Ulaya kwenyewe
waliacha, mtu wa design hiyo ni mtu ambaye hata nauli ya kwenda studio
hana, ana matatizo.”
“Angekuja
kuongea na mimi ningemwambia andika lyrics hizi ni poa zaidi hata
wananchi watakuelewa.Siwezi kumjibu Nikki Mbishi hata siku moja. Yeye
anahustle ili atoke kwenye muziki lakini mimi mwenzake naishi bila
muziki so mimi naweza nikamlea yeye na akaishi vizuri, nikamtengenezea
nywele zake anazosuka, nikamkodishia na salon kwenda kusuka kila
anapohitaji. Sio mara ya kwanza, alishaniimba kabla ya hapa mimi
nikachukulia poa,” alisisitiza Ney wa Mitego.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment