HATIMAYE MATUMAINI ATUA DAR.....ANGALIA PICHA


Matumaini (katikati) akisaidiwa na wasanii wenzake muda mfupi baada ya kutua.
    Bi. Mwenda akiwa amembeba Matumaini mgongoni.
Matumaini (kulia) akiwa na Bi. Mwenda (wa pili kushoto) na anayefuata (kushoto) ni msanii mwenzake Kiwewe wakisubiri gari la kumpeleka hospitali.
  Askari wakiwaelekeza wasanii kukaa upande mmoja ili apate hewa.
Matumaini akiwa amebebwa mgongoni na msanii mwenzake, Mariam Athuman ‘Kalunde’ akimpeleka kwenye gari.
Mama mkubwa wa Matumaini, Bi. Elizabeth (kushoto) na Matumaini (katikati) wakiwa ndani ya gari tayari kuelekea hospitali ya Amana.
Rais wa Shirikisho la Filamu nchini (TAFF), Simon Mwakifwamba akizungumza na wasanii maeneo ya Amana wakati Matumaini akiwa kwa daktari.
-----------
MSANII wa vichekesho ambaye alikuwa nchini Msumbiji, Tumaini Mwakibibi ‘Matumaini’ jana alipokelewa na wasanii wenzake kibao baada ya kutua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar akiwa hoi kutokana na kusumbuliwa na maradhi kwa muda mrefu.
Matumaini alitua uwanjani hapo jana majira ya saa 9:30 alasiri ambapo kutokana na hali yake kuwa mbaya wasanii walimbeba mgongoni na kumfikisha kwenye gari ambapo walimpeleka moja kwa moja hospitali ya Amana alikolazwa mpaka sasa akiendelea kupatiwa matibabu.


Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment