MWANA FA AANZISHA LIFE LINE INC

 

"niliona naweza kutoa mkono sasa, nimefanya mziki kwa mda mrefu na siwezi kumsaidia kila mmoja anaefanya mziki, kuna watu wanavipaji vinapotea mtaani huku, na nikaona naweza kufanya kitu, kwahiyo tutakua very selective, maana hatutaki kuwa na watu wengi kwenye lebo tukashindwa kusambaza kazi zao
tutachagua wawili watatu ambao tutaona vipaji vyao vinajitosheleza na kuwasimamia haitatupashida, maua ndio ameanza sema kuna wengine wawili watatu mnawajua ila maua tumeona ndio wakati wake, na muda haujafika wa sisi kuwataja na kuanza nao kazi rasmi hadharani, bado tunafanya kichinichini"

"lebo ina kama mwaka hivi lakini tunaendesha shughuli kichinichini, tunajaribu  ku scout watu, kupanga mambo yetu, kusajili kampuni yaani utaratibu wa nyuma kabla mziki haujaskika na mtu wa kwanza kutoka ni maua kwasababu muda wake umefika na niwakati wa kipaji chake kukipeleka mbele na sio cha kukilazia damu au kulala nacho"amesema  FA baada ya kuulizwa lebo imekuwepo kwa muda gani
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment