"niliona naweza kutoa mkono sasa, nimefanya mziki kwa mda mrefu na
siwezi kumsaidia kila mmoja anaefanya mziki, kuna watu wanavipaji
vinapotea mtaani huku, na nikaona naweza kufanya kitu, kwahiyo tutakua
very selective, maana hatutaki kuwa na watu wengi kwenye lebo
tukashindwa kusambaza kazi zao
tutachagua wawili watatu ambao tutaona
vipaji vyao vinajitosheleza na kuwasimamia haitatupashida, maua ndio
ameanza sema kuna wengine wawili watatu mnawajua ila maua tumeona ndio
wakati wake, na muda haujafika wa sisi kuwataja na kuanza nao kazi rasmi
hadharani, bado tunafanya kichinichini""lebo ina kama mwaka hivi lakini tunaendesha shughuli kichinichini, tunajaribu ku scout watu, kupanga mambo yetu, kusajili kampuni yaani utaratibu wa nyuma kabla mziki haujaskika na mtu wa kwanza kutoka ni maua kwasababu muda wake umefika na niwakati wa kipaji chake kukipeleka mbele na sio cha kukilazia damu au kulala nacho"amesema FA baada ya kuulizwa lebo imekuwepo kwa muda gani
0 comments:
Post a Comment