IKIWA ni takribani siku siku 47 tangu alipofariki staa wa filamu za Kibongo, Juma Kilowoko ‘Sajuki’, kuna madai kuwa tayari visa vimeanza kati ya mkewe Wastara Juma na mama yake mzazi yaani mkwewe, Ijumaa Wikienda limetonywa.
Wastara Juma.
Kwa mujibu wa chanzo makini, mama Sajuki amekuwa akidaiwa kumfuatilia
Wastara kwa kila anachokifanya hadi kufikia hatua ya kuwaambia watu
wamchunguze.Chanzo hicho kilidai kuwa Wastara na mama Sajuki walifikia hatua ya kurushiana maneno mbele za watu huku ulemavu wa mjane huyo wa Sajuki ukitajwatajwa.
“Unaambiwa wakija watu kumuombea dua Wastara na kumwambia atapata mwanaume mwingine, mama Sajuki anashindwa kuvumilia na kujikuta akiangua kilio,” kilidai chanzo hicho.
0 comments:
Post a Comment