WEMA NA ANTI EZEKIEL WAKATA MAUNO MTAANI

Na Imelda Mtema
MASTAA wakali wa sinema za Kibongo, Wema Sepetu na Aunt Ezekiel walifunga mtaa na kuanza kukata mauno kinomanoma na kusababisha umati wa watu uwazunguke.
Aunt Ezekiel wakikata mauno.  
Mpango mzima ulitokea hivi karibuni katika arobaini ya mtoto wa dada yake Wema iliyofanyika Sinza Kwa - Remmy, jijini Dar ambapo Aunt pamoja na baadhi ya wasanii walifika kusherehekea sherehe hiyo ya kumtoa mtoto.
...Warembo hao wakiwa katika pozi.
Awali, Wema alionekana akimtunza fedha pamoja na mikufu ya dhahabu yenye thamani kubwa na ilipoisha sherehe ya maulid ndipo mastaa hao waliwasha muziki na kuanza kulisakata rumba.
 “Sisi tumecheza tumefurahi tu hawa waliofunga mtaa kututazama watakuwa wanataka kuona mavituzi yetu,” alisema Wema. 
 ...Wakizidi kumwaga radhi.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment