Abdul ‘Diamond Platnumz’ akiwa na aliyewahi kudaiwa kuwa mpenzi wake, Jokate Mwegelo.
Akizungumza na Ijumaa Wikienda katika mahojiano maalum alipobanwa
kuhusiana na uhusiano wa wapenzi hao huku ikifahamika kuwa Penny alikuwa
shosti wake, Jokate ambaye ni Miss Tanzania namba 2, 2006/07 alisema
kwamba yeye na mrembo huyo walikuwa washikaji tu na wala hawakuwa na
urafiki wa karibu kama baadhi ya watu wanavyoamini.
Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ akiwa na demu wake mpya, Penniel Mungilwa ‘Penny’.
Jokate ambaye pia ni mtangazaji wa Runinga
ya Channel O alifunguka kuwa anawatakia kila la heri na baraka zote
Diamond na Penny katika uhusiano wao mpya wa kimapenzi endapo tu
watakuwa wamependana na kuridhiana kwa dhati.
“Japokuwa sipendi kumuongelea Diamond lakini ukweli sioni tatizo kwa wao kupendana, mimi naona poa tu,” alifunguka Jokate ambaye pia ni bonge la mwigizaji.
Kabla ya kutoka kimapenzi na Penny ambaye naye ni mtangazaji wa Runinga ya DTV, Diamond aliwahi kuviteka vyombo vya habari akiripotiwa kuwa na Jokate, kabla ya mambo kwenda mrama.

0 comments:
Post a Comment