RAIS
wa Jamuhuri wa Muungano wa Tanzania Dk.Jakaya Mrisho Kikwete amehaidi
kuwasaidia Mamlaka ya Vitambulisho (NIDA) kwa kuiwezesha kupata
fedha kwa ajili Vitambulisho vya Taifa ili kabla ya uchaguzi wa
mwaka 2015 watu wote watakuwa na vitambulisho vya Taifa vitakavyo tumika
katika uchaguzi huo.
Aidha Rais Kikwete aliitaka NIDA kutoa vitambulisho kwa watu
wanaotakiwa na kuchukulia hatua za kisheria wale watakaokiuka sheria ya
usajili wa vitambulisho hivyo.
Kauli hiyo ilitolewa leo na Rais Kikwete wakati uzinduzi wa mfumo
wa usajili na utambuzi wa watu kitaifa na utoaji wa vitambulisho hivyo
uliofanyika katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.
Rais Kikwete aliwataka wananchi kuwa wazalendo kwa kutoa taarifa
zao kwa uaminifu na kutoa ushirikiano ili kurahisisha zoezi hilo.
Aliwataka viongozi wa dini, serikali na waandishi wa habari kuwa
mstari wa mbele katika kuwahamasisha wananchi kutoa ushirikiano huo.
Naye Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dk. Emmanuel Nchimbi
alisema ni muhimu kuwa na vitambulisho vya Taifa kwani ni jambo la
msingi ambalo litaweza kuwa na manufaa makubwa kwa kuunganisha mifumo
mikubwa ya usajili ya kitaifa.
Baadhi ya mifumo hiyo ni kama Mfumo wa usajili wa kodi(TRA), Mfumo
wa vizazi na vifo(RITA),Mfumo wa pasi za kusafiria(UHAMIAJI),Mfumo wa
POLISI, Mifumo ya mawasiliano yasimu(Vodacom,Tigo,Zantel,Airtel,TTCL),Mfumo wa Taarifa za kiutumishi na
Mishahara Serikalini, Mifumo ya Hifadhi za kijamii,Mifumo ya Taasisi za
kifedha,Mifumo ya udahili ya Wanafunzi(Loan Board),n.k.
Mkurugezi Mkuu wa NIDA, Dickson Maimu alizitaja changamoto
mbalimbali za kiutendaji zikiwemo wananchi kukosa viambatanisho muhimu
vya kuwatambulisha,uhakiki wa taarifa za uraia,Uhakiki wa taarifa za
makazi,Upungufu wa vifaa na Rasilimali watu.
Aliyataja mahitaji halisi ya zoezi hilo kuwa ni vifaa vya
kuchukulia alama za vidole, picha saini takribani 12,000, rasilimali
watu wa muda 114,000 na wakudumu 3000 ili kukukamilisha mpango huo kwa
muda utaotakiwa.
0 comments:
Post a Comment