BAADA ya mwanaye kutoka mahabusu kwa dhamana, mama wa msanii wa filamu
Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’, Lucresia Karugila, hivi karibuni
alinaswa akimpa mbinu mama wa msanii Kajala Masanja zitakazomsaidia
kumuokoa mwanaye.
Akina mama hao walinaswa na paparazi wetu kwenye
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki
iliyopita ambapo Kajala na mumewe, Faraja Chambo walifikishwa kwa ajili
ya kujitetea kwenye kesi inayowakabili ya kutakatisha fedha haramu.
Katika
tukio hilo, mama Lulu ndiye aliyeanza kufika mahakamani hapo na baada
ya muda, alitokea mama Kajala ambapo walisimama chobingo na watu
waliokuwa karibu yao walidai mama Lulu alikuwa akimpa mwenzake mbinu za
kumwezesha kumuokoa mwanaye na kesi hiyo.
“Naona mama Lulu anampa
mwenzake mbinu za kumuokoa Kajala ila amefanya la maana sana kuja kumpa
kampani na kwa uzoefu wake wa mahakamani anaweza kumsaidia,” alidai mama
mmoja aliyekuwa karibu yao.
Hata hivyo, wazazi hao walisitisha
mazungumzo baada ya Kajala na mumewe kutolewa chumba cha mahabusu na
kupandishwa kizimbani ambapo Wakili wa Serikali, Renald Swai
aliiahirisha kesi hiyo hadi Februari 12 (kesho) baada ya kupokea udhuru
kutoka kwa hakimu aliyetakiwa kusikiliza kesi hiyo, Sundi Fimbo.
Baada
ya kuahirishwa kwa kesi hiyo, mama Lulu aliendelea kuwa karibu na mama
Kajala ila kilichowatawanyisha kilikuwa ni mwanga wa kamera ya paparazi
wetu.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment