Kwa habari zilizotufikia hivi punde zinasema Papa Benedict XVI (85) ajiuzulu wadhifa wake.
Ikiwa ni mara ya kwanza kwa kiongozi wa
wadhifa huo kufanya hivyo kwa miaka 600 iliyopita, Papa Benedict XVI
amejiuzulu kwa sababu aliyoitoa mwenyewe kuwa ni kutokana na umri.
Na ataachia madaraka February 28 na Papa
mwingine atachaguliwa Machi. ''Baada ya kutafakari umri wangu sasa
hainiruhusu kuendelea katika wadhifa huu kutokana na mabadiliko ya
kiimani kwa mujibu wa Mtakatifu Peter...'' alisema Mtakatifu Benedict
(85).
Papa
wa mwisho kujiuzulu alikua ni Papa Gregory ambaye alijiuzulu mwaka 1415
kutokana na mgawanyiko wa kidini katika nchi za magharibi
0 comments:
Post a Comment