1.
Nitakupa kila unachotaka. Hivi huwa mnajua makosa yanayozaa kshfa
mnazowapa sasa wasichana kuwa wanapenda pesa chanzo ni nyinyi? Kama
unamuahidi msichana utampa kila atakachotaka akija kukuambia ana shida
ya laki tano kwanini umshangae na kumuona anapenda pesa? Inawezekana
ikawa amekukubalia kutokana na hili.
2. Usimueleze ukweli juu ya
idadi ya wasichana uliowahi kuwa nao hii husababisha kujifikiria mara
mbili msichana aliyekupenda kweli huogopa kuingia katika mlolongo wa
foleni ya wasichana na kuongeza idadi katika wasichana watakaopita kama
wenzake. Msichana humuona mvulana wa aina hii kamahajatulia ama ni mtu
wa kuchezea wasichana itakuwia vigumu kumshawishi
3.
Usitumie pesa kama kigezo cha kumpata. Kuna wavulana ambao hutumia
nguvu ya pesa kumlaghai msichana wakidhani kuwa wakifanya hivyo ndio
watapendeka lakini hii si sawa kwa kuwa mwanamke anaweza akakuchukulia
mtu wa kukuchuna hata kama alikuwa na nia ya kukupenda kweli.
4.
Usimdanganye hali halisi yamaisha ya nyumbani kwenu usiogope ubovu wa
nyumbani kwenu ikiwa ni mafukara wa hali ya juu usione aibu kumueleza
ukweli kwa sababu atakapokukubali ukiwa umemdanganya kuwa nyumbani kwenu
kuna gorofa halafu asilikute, msichana atakuona wewe ni muongo na huna
lolote utakalomueleza akakuamini
5. Usimueleze msichana umempenda
kwasababu yeye ni mzuri akitembea anakuvutia unaipenda sauti yake au
akicheka unapenda sana kwa sababu akikuuliza je nisingekuwa hivyo ina
maana usingenipenda je ungemjibu nini unalo? Sasa sikia wasichana
wanapenda kupendwa kweli hawapendi kuchezewa hawapendi kudanganywa hivyo
utakapomfuata kuwa makini na utakachomueleza mpaka akuelewe.
About Unknown
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment